BREAKING NEWS

[5]

MAISHA NA MAHUSIANO

By Noel Peter.
Jambo muhimu la kujua ni hili lifuatalo katika kujenga maisha yenye furaha amani na mahusiano mazuri kati yetu wenyewe,Sisi  na Jirani zetu na pia kati yetu na MUNGU.


:MPENDE BWANA MUNGU WAKO.
Deuteronomy 6:5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

Deuteronomy 11:1 Kwa ajili hii mpende Bwana, Mungu wako, na kushika sikuzote mausia yake, na amri zake, na hukumu zake, na maagizo yake. 


Nani Huyo au nini hicho kinachukua nafasi ya MUNGU Kwenye Moyo wako na maisha yako mpaka umepunguza au humpendi Mungu Muumba wako?.Kumbuka Mungu anakupenda sana anasema:

Joshua 23:11 "Jihadharini nafsi zenu, basi, ili mmpende Bwana, Mungu wenu."

Zaburi 31:23 "Mpendeni Bwana, Ninyi nyote mlio watauwa wake. Bwana huwahifadhi waaminifu, Humlipa atendaye kiburi malipo tele" Hili ni muhimu sana BWANA YESU KRISTO anasisitiza hivyo usipuuzie hata kidogo..

Matthayo 22:37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.

Marko 12:30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.

Luka 10:27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.


MPENDANE "LOVE ONE ANOTHER"
Rafiki yangu mmoja alisema "I LOVE WHAT GOD LOVES AND HATE WHAT GOD HATES" Kwa maana ya kwamba "NINAPENDA KILA MUNGU ANACHOPENDA NA NINACHUKIA KILE MUNGU ANACHOCHUKIA".Mungu anapenda kila mtuUlimwengu mzima  mtu wa kila hali na kila namna kwani "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.~John 3:16 " MUNGU ANACHUKIA DHAMBI NA NA ANAWAPENDA WANADAMU WOTE NDIO MAANA ALIAMUA KUMTOA KRISTO MSALABANI AFE KWAAJILI YA DHAMBI ZETU ZOTE.Unapendwa! Unapendwa! Unapendwa! MUNGU anakupenda,Hivyo Hivyo wapende na wengine
Yohana 13:34 " Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo."

1John 4:8 "Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo"

1Corinthians 13:1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

1Corinthians 13:2 "Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi."

1Corinthians 13:3 "Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.".

TAFUTA AMANI NA MUNGU NA PIA AMANI NA WATU WOTE.
Hebrews 12:14 "Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;"

Proverbs 8:17 Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
 

Isaiah 55:6 Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;

Amos 5:6 Mtafuteni Bwana, nanyi mtaishi; asije akawaka kama moto katika nyumba ya Yusufu, nao ukateketeza, asiwepo mtu awezaye kuuzima katika Betheli.



          

 June 2014.









MAISHA NA MAHUSIANO  MAISHA NA MAHUSIANO Reviewed by Unknown on 7:23 PM Rating: 5

Sora Templates