BREAKING NEWS

[5]

SAUTI YA NENO










SIKIA NENO LA BWANA.
We carry Good news of JESUS CHRIST to all people on earth/Habari njema za YESU KRISTO kwa watu wote waishio duniani. Your situation/status upon any obstacle has nothing to do with the ability to tackle such problem, but what matters is your recognition of the power of Jesus Christ and your WILLINGNESS to accept him and allow him to tackle any problem for you! Get connected to Jesus NOW!

Warumi 8:1-3
Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. 3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;

Mathayo 11:28-30
"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."

1Yohana 4:10
Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.

warumi 10:9
"Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka."

Matendo ya Mitume 4:12

"Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."


Yohana 5:24

 "Amin,amin nawaambia,yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele;wala haingii hukumuni,bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani,...(mstr 25). saa inakuja,na sasa ipo,wafu watakapoisikia sauti ya mwana wa mungu,na wale waisikiao watakuwa hai"
 
Bwana anasema:
Mark 16:15
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Mathayo 28:18-20
"Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
 .Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.


 
SAUTI YA NENO SAUTI YA NENO Reviewed by Unknown on 7:25 PM Rating: 5

Sora Templates