SAA YA WOKOVU NI SASA!. NJOO KWA YESU KRISTO MWOKOZI.
Matthayo 11:28
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Umempa Yesu kristo maisha yako? Unamwamini? Je umempokea binafsi kama BWANA na mwokozi wa maisha yako? Lini unaenda kumpa kristo maisha? Kumbuka kila mtu anamhitaji kristo
kama anavyosema katika Biblia kwenye mistari ifuatayo:
Warumi 3:23
"kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;"
Warumi 5:12
Warumi 5:12
"Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;"
wote tumefanya dhambi.Lakini kwa kifo chake YESU KRISTO pale msalabani alilipa deni na adhabu ya dhambi ya kila mwanadamu kwa vizazi vyote.Hivyo unachotakiwa kufanya ni kumwamini Kristo na kumpokea kama mwokozi wako
Matendo ya Mitume 4:12
"Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."
Lini unatakiwa ufanye uamuzi huu muhimu?
Hebu MUNGU na aseme nawe kupitia maneno yake ambayo ni amina na kweli anasema:
Warumi 13:11
Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini
2Wakorintho 6:2
2Wakorintho 6:2
"Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa"
Biblia inaonya kuwa "tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa" yaani wakati huu unaposoma hapa ndio wakati wako wa kutubu na kumgeukia Mungu kwa njia ya kristo kama bado haujafanya hivyo kwani huu ni uamuzi ambao kila mwanadamu lazima aufanye.Mungu ana kalenda yenye miaka mingi lakini kwenye swala la kuukiri wokovu wa kristo wakati ni sasa..Ninakuomba umpe kristo maisha yako,ili hata kama ukifa muda wowote akupokee na uishi naye milele.
unatakiwa kufanya nini ili upate kuokoka?
Hebu tuone hapa jinsi maandiko yanavyotupa jibu:
Matendo ya mitume 2:37-40
"Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.
Matendo ya Mitume 16:30-31
" kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako."
Inawezekana nawe unajiuliza ya kwamba unawezaje kupokea kipawa hiki cha Mungu cha wokovu kwa njia ya Yesu Kristo ukisema na kuuliza moyoni "Tutendeje, ndugu zetu?".Jibu linapatikana unatakiwa kufanya yafuatayo:
1.Tubu dhambi zako zote ulizotenda mbele ya Mungu kwa kumwambia kwamba umekosa na muombe akusamehe na akupe nguvu ya kushinda hiyo dhambi ili usije ukaanguka tena.atakusamehe na kukupokea ikiwa utafanya hivyo kwa moyo wako wote na kwa imani.
2.Mwamini Bwana Yesu na mkaribishe kwenye moyo wako na maisha yako.Ni Yesu pekee ndio mwokozi wa ulimwengu na hakuna njia nyingine yoyote ile ya kumfikia Mungu isipokuwa kristo Yesu hata anasema mwenyewe "Yohana 14:6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi."
3.Liitie Jina la Yesu
Tunaokolewa kwa kupitia jina moja tu! vizazi vyote na jamii yote ya mwanadamu tunaokolewa kwa jina la yesu.JINA LA YESU NDILO LILILOBEBA WOKOVU WA KILA MWANADAMU Nsema katika Mathayo 1:21 "Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao." pia anasema
Matendo ya Mitume 2:21 "Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa." Warumi 10:13 " kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka."
Usiache nafasi hii ikupite bila ya kuliitia jina la Yesu hakika litafanya kazi kwako!
Liitie Jina la YESU KRISTO kwanjia ya maombi toka moyoni mwako na mwombe Bwana akusamehe dhambi zako zote nawe utaokoka sasa! hivyohivyo ulivyo Kristo anakupenda na kamwe hatakutupa ukimwendea.kwa ahadi hii hakikisha umefanya uamuzi wa kumpa kristo maisha yako.
John 6:37
"Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe."
John 6:35
"Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe."
Biblia katika Yohana 12:44-50 inasema:
"Naye Yesu akapaza sauti, akasema,
Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka.45 Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka.
46 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani. 47 Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.
48 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.49 Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.
50 Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.
Bado unamkataa YESU na maneno yake? lini utamkubali na kumwamini?.kumbuka YESU Ni MWOKOZI na saa ya wokovu ni sasa!.

Sali sala hii fupi toka moyoni Ukimtazama na kuamini kwamba Mungu anakusikia kama umeamua kumwamini yesu
na unataka atawale maishani mwako,akupe furaha amani na msamaha wa dhambi na
akufanye kuwa mwana wa mungu sawasawa na alivyoahidi omba ukisema:
"BWANA YESU NINAKUJA KWAKO MIMI NI MWENYE DHAMBI NINAOMBA UNISAMEHE NA KUNIOKOA.KARIBU KWENYE MAISHA YANGU NA MOYO WANGU,UNISAMEHE MAOVU YANGU YOTE,UNIOSHE NA KUNITAKASA.KUANZIA SASA MIMI NI WAKO.NINAKUSHUKURU KWA KUWA ULIKUFA MSALABANI KWA AJILI YA DHAMBI ZANGU NA KWA KUNIPOKEA.SASA NIMEOKOKA.MIMI NI MWANA WA MUNGU,Amen"
Amini kwamba umeokoka,Kristo ameingia ndani yako,wewe sasa umekuwa kiumbe kipya kwani anasema katika "2Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya." pia ahadi hii inakuhusu sana anasema "Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;"
Mambo ya kuzingatia:
MUNGU wa mbinguni ni Baba yako.sema naye kwanjia ya maombi na sikia kutoka kwake kwanjia ya kusoma Biblia.Kama unapata shida kusoma Biblia nakushauri anza na kitabu cha Yohana Mtakatifu,ukimaliza Soma Warumi halafu malizia Biblia yote katika hali ya maombi na kumwamini Mungu utashangaa kuona jinsi Mungu anavyokupenda na alivyo kuahidia mambo mazuri mno katika ulimwengu wa sasa na ule unaokuja baada ya kufa.Omba usiache.
Nenda kanisani ukamwabudu Mungu wako siku zako zote.Ubarikiwe na Bwana pia usisite kumwambia mwingine Baba,Mama,Mjomba,Kaka,Dada,Rafiki,Boyfriend,Girlfriend Habari hizi kwamba Yesu anaokoa na ya kuwa wewe mwenyewe umempokea na amekusamehe dhambi zako kama alivyoahidi na ukifa sasa utaurithi uzima wa milele.
"BWANA akubariki pia na alibariki NENO lake!

Reviewed by Unknown
on
10:12 PM
Rating: