BREAKING NEWS

[5]

MTU AKIWA NDANI YA KRISTO


Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! Yamekuwa mapya(2Wakorintho 5:17)

Yeye mwenyewe (Yesu Kristo) alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti; ili tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na KWA KUPIGWA KWAKE MLIPONYWA(1Petro 2:24)



Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye KATIKA YEYE TUNA UKOMBOZI YAANI, MSAMAHA WA DHAMBI.(Wakolosai 1:13,14).


Kumbuka;


Warumi 8:1-2  
Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. 2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Yohana 3:18 
Amwaminiye yeye (YESU KRISTO) hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

Yohana 3:36 
Amwaminiye Mwana (YESU KRISTO ) yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.



Ni uamuzi wako!

Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.Matendo 16:31

Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka Warumi 10:9


Ikiwa unasikia sauti ya MUNGU ndani ya moyo wako ikikuambia unahitaji kumpokea YESU KRISTO basi fuatana nami kwa kuomba kwa imani maombi haya;

BWANA YESU,NAJA KWAKO (MIMI) KAMA NILIVYO,NIMETAMBUA YA KWAMBA MIMI NI MWENYE DHAMBI.NIMETAMBUA YA KWAMBA NI WEWE TU UNAYEWEZA KUNISAMEHE NA KUNITAKASA.NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE.
NAOMBA ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU,NA KULIANDIKA KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE.
NAYAKABIDHI MAISHA YANGU KWAKO,UNILINDE NA MWOVU SHETANI.
NAJITOA KWAKO KUANZIA LEO/SASA,UNIFANYE KUWA KIUMBE KIPYA NA UNITUMIE KAMA UPENDAVYO.
AHSANTE KWA KUNIKUBALI
AMEN.









MTU AKIWA NDANI YA KRISTO MTU AKIWA NDANI YA KRISTO Reviewed by Unknown on 1:30 AM Rating: 5

Sora Templates