BREAKING NEWS

[5]

ANZISHA UHUSIANO BINAFSI NA MUNGU KWA NJIA YA YESU KRISTO.

Mithali 8:17 "
Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona."

Isaiah 55:6 
Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;

Waebrania 12:14 
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

Yohana 3:16 
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.


UNAPENDWA NA MUNGU!
Wewe ni wa thamani sana hata kama haujui! Mungu anakupenda! Alimtoa kristo akafa msalabani ili kulipa deni la dhambi zetu zote tulizofanya  na kumwasi mungu kwani.Thamani ya ko ni Damu ya Mwana wa Mungu isiyo na ila wala dhambi...Halleluyah,Unapendwa!

1Peter 1:18-19 "18 
"Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
 20 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; 21 ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu."
Umeamini? Unapendwa! Kristo alikuwepo miaka mingi mingi milele yote,lakini alifunuliwa kwajili yetu sote,mimi na wewe, sisi ni sababu hasa ya kristo kuja ulimwenguni. Unapendwa!



UNAMHITAJI YESU KRISTO,FANYA UAMUZI SASA UMKARIBISHE MAISHANI MWAKO.
Hizi ndio sababu kwa nini unamhitaji Yesu kristo:

Warumi 3:23 "kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;"  

Warumi 5:12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;

Maandiko yanaendelea kueleza juu ya huyu Yesu kristo inasema katika "Warumi 5:18-19
 18 Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.  19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki."

UNATAKIWA KUFANYA NINI?
Hebu tuone hapa jinsi maandiko yanavyotupa jibu:

Matendo ya mitume 2:37-40
"Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.

Matendo ya Mitume 16:30-31
" kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako."

Inawezekana nawe unajiuliza ya kwamba unawezaje kupokea kipawa hiki cha Mungu cha wokovu kwa njia ya Yesu Kristo ukisema na kuuliza moyoni "Tutendeje, ndugu zetu?".Jibu linapatikana unatakiwa kufanya yafuatayo:

1.Tubu dhambi zako zote ulizotenda mbele ya Mungu kwa kumwambia kwamba umekosa na muombe akusamehe na akupe nguvu ya kushinda hiyo dhambi ili usije ukaanguka tena.atakusamehe na kukupokea ikiwa utafanya hivyo kwa moyo wako wote na kwa imani. Pia  
"Mithali 28:13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema."

2.Mwamini Bwana Yesu na mkaribishe kwenye moyo wako na maisha yako.Ni Yesu pekee ndio mwokozi wa ulimwengu na hakuna njia nyingine yoyote ile ya kumfikia Mungu isipokuwa kristo Yesu hata anasema mwenyewe 

"Yohana 14:6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi."

3.Liitie Jina la Yesu
Tunaokolewa kwa kupitia jina moja tu! vizazi vyote na jamii yote ya mwanadamu tunaokolewa kwa jina la yesu.JINA LA YESU NDILO LILILOBEBA WOKOVU WA KILA MWANADAMU 

Imesemwa katika Mathayo 1:21 "Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao." pia anasema
Matendo ya Mitume 2:21 "Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa." Warumi 10:13 " kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka."

Usiache nafasi hii ikupite bila ya kuliitia jina la Yesu hakika litafanya kazi kwako! 
Liitie Jina la YESU KRISTO kwanjia ya maombi toka moyoni mwako na mwombe Bwana akusamehe dhambi zako zote nawe utaokoka sasa! hivyohivyo ulivyo Kristo anakupenda na kamwe hatakutupa ukimwendea.kwa ahadi hii hakikisha umefanya uamuzi wa kumpa kristo maisha yako.

Yohana 6:37 
"Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe."

Yohana 6:35 
"Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe."

Biblia katika Yohana 12:44-50 inasema:
"Naye Yesu akapaza sauti, akasema,
Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka.45 Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka.
46 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani. 47 Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.
48 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.49 Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.
50 Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.

Je nawewe ni miongoni ambao bado unamkataa YESU na maneno yake? lini utamkubali na kumwamini?.kumbuka YESU Ni MWOKOZI WAKO,AMEKUFIA MSALABANI na  saa ya wokovu ni sasa FANYA MAAMUZI YA KUMFUATA KRISTO!.



Sali sala hii fupi toka moyoniUkimtazama na kuamini kwamba Mungu anakusikia kama umeamua kumwamini yesu na unataka atawale maishani mwako,akupe furaha amani na msamaha wa dhambi na akufanye kuwa mwana wa mungu sawasawa na alivyoahidi omba ukisema:
"BWANA YESU NINAKUJA KWAKO MIMI NI MWENYE DHAMBI NINAOMBA UNISAMEHE NA KUNIOKOA.KARIBU KWENYE MAISHA YANGU NA MOYO WANGU,UNISAMEHE MAOVU YANGU YOTE,UNIOSHE NA KUNITAKASA.KUANZIA SASA MIMI NI WAKO.NINAKUSHUKURU KWA KUWA ULIKUFA MSALABANI KWA AJILI YA DHAMBI ZANGU NA KWA KUNIPOKEA.SASA NIMEOKOKA.MIMI NI MWANA WA MUNGU,
Amen"
Sasa ndo umeokoka ivyo, Kristo ameingia ndani yako,wewe sasa umekuwa kiumbe kipya kwani anasema katika 
"2Wakorintho 5:17 
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya." pia ahadi hii inakuhusu sana anasema "

Yohana 1:12
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

Mambo ya kuzingatia: 




1. Zungumza na Mungu kwa maombi kila siku (Yohana 15:7)
2. Soma Neno la Mungu (Biblia) kila siku (Matendo ya Mitume 17:11)
3. Mruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-25; Warumi 8:14-17)
4. Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1Petro 5:7; Zekaria 4:6)
5. Usiache kukusanyika na kushirikiana na wengine waliompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao kama wewe ili uimarike zaidi (Waebrania 10:25)
 


Unapendwa!
MUNGU wa mbinguni ni Baba yako.sema naye kwanjia ya maombi na sikia kutoka kwake kwanjia ya kusoma Biblia.Kama unapata shida.
Jenga mazoea ya Kusoma Biblia nakushauri anza na kitabu cha Yohana Mtakatifu,ukimaliza Soma Warumi halafu malizia Biblia yote katika hali ya maombi na kumwamini Mungu utashangaa kuona jinsi Mungu anavyokupenda na alivyo kuahidia mambo mazuri mno katika ulimwengu wa sasa na ule unaokuja baada ya kufa.Omba usiache.












ANZISHA UHUSIANO BINAFSI NA MUNGU KWA NJIA YA YESU KRISTO. ANZISHA UHUSIANO BINAFSI NA MUNGU KWA NJIA YA YESU KRISTO. Reviewed by Unknown on 7:08 PM Rating: 5

Sora Templates