BREAKING NEWS

[5]

JIANDAE YESU ANAKUJA



BWANA YESU ANASEMA;

ufunuo wa Yohana 22:7 
Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.

ufunuo wa Yohana 22:12 
Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

NJOO SASA ANAKUSUBIRI.
Yohana 6:37 
"Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe."

YESU KRISTO YU KARIBU SANA KURUDI KUCHUKUA KANISA LAKE WALA HACHUKUI MAJENGO BALI NI WALE WALIOTUBU DHAMBI ZAO NA MAASI YAO.WALIO AMUA KUYAKANA MAISHA YA DHAMBI NA ANASA ZA DUNIA HII NA KUAMUA KUMFUATA YESU KRISTO NA KUISHI MAISHA YA USAFI NA UTAKATIFU.


Sali sala hii fupi toka moyoni Ukimtazama na kuamini kwamba Mungu anakusikia kama umeamua kumwamini yesu na unataka atawale maishani mwako,akupe furaha amani na msamaha wa dhambi na akufanye kuwa mwana wa mungu sawasawa na alivyoahidi na akuweke Tayari kwa kumpokea YESU KRISTO Pale atakaporudi, omba ukisema:

"BWANA YESU NINAKUJA KWAKO MIMI NI MWENYE DHAMBI NINAOMBA UNISAMEHE NA KUNIOKOA.KARIBU KWENYE MAISHA YANGU NA MOYO WANGU,UNISAMEHE MAOVU YANGU YOTE,UNIOSHE NA KUNITAKASA.KUANZIA SASA MIMI NI WAKO.NINAKUSHUKURU KWA KUWA ULIKUFA MSALABANI KWA AJILI YA DHAMBI ZANGU NA KWA KUNIPOKEA.SASA NIMEOKOKA.MIMI NI MWANA WA MUNGU,Amen"
JIANDAE YESU ANAKUJA JIANDAE YESU ANAKUJA Reviewed by Unknown on 2:28 AM Rating: 5

Sora Templates