BREAKING NEWS

[5]

SISI JE! TUTAPATAJE KUPONA? TUSIPOJALI WOKOVU MKUBWA NAMNA HII

Kisha NIKAONA KITI CHA ENZI, KIKUBWA, CHEUPE, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.


NIKAWAONA WAFU, WAKUBWA KWA WADOGO, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na VITABU VIKAFUNGULIWA; na KITABU KINGINE KIKAFUNGULIWA, AMBACHO NI CHA UZIMA; na hao WAFU WAKAHUKUMIWA KATIKA MAMBO HAYO YALIYOANDIKWA KATIKA VILE VITABU, sawasawa na matendo yao.



Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. WAKAHUKUMIWA KILA MTU KWA KADIRI YA MATENDO YAKE.



NA IWAPO MTU YE YOTE HAKUONEKANA AMEANDIKWA KATIKA KITABU CHA UZIMA, ALITUPWA KATIKA LILE ZIWA LA MOTO.

(Ufunuo 20:10-15)


Sisi je! Tutapataje kupona, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; (Waebrania 2:3)



Ndugu yangu na Rafiki yangu Maandiko yanasema;

Hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana HAPANA JINA JINGINE chini ya mbingu WALILOPEWA WANADAMU LITUPASALO SISI KUOKOLEWA KWALO. (Matendo 4:12)


Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; UZIMA HUU UMO KATIKA MWANAWE. (1Yohana 5:11)



Sasa Unaniuliza, yanipasa nifanye nini ili nipate kuokoka?

Jawabu langu ni hili;
MWAMINI BWANA YESU, NAWE UTAOKOKA  PAMOJA  NA  NYUMBA YAKO. (Matendo 16:31)


Kwani yeye mwenyewe anasema;

Amin, amin, nawaambia, YEYE ALISIKIAYE NENO LANGU NA KUMWAMINI YEYE ALIYENIPELEKA YUNA UZIMA WA MILELE; wala HAINGII HUKUMUNI, bali AMEPITA KUTOKA MAUTINI KUINGIA UZIMANI. (Yohana 5:24)


Kuna leo kuna Kesho, Hakuna ajuaye, Amua mustakabali wa maisha ya baadaye ya kwa kutubu dhambi zako zote na uovu wako wote mbele za MUNGU na Amua kumwamini na kumpokea YESU KRISTO kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako!



Kumbuka;

Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; (Yohana 1:12)
SISI JE! TUTAPATAJE KUPONA? TUSIPOJALI WOKOVU MKUBWA NAMNA HII SISI JE! TUTAPATAJE KUPONA? TUSIPOJALI WOKOVU MKUBWA NAMNA HII Reviewed by Unknown on 6:28 AM Rating: 5

Sora Templates