Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. #Warumi 5:8
kwa maana PENDO LA MUNGU limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. #Warumi 5:5
Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. MUNGU NI UPENDO, NAYE AKAAYE KATIKA PENDO, HUKAA NDANI YA MUNGU, na Mungu hukaa ndani yake. #1Yohana 4:16
SISI TWAPENDA kwa maana YEYE ALITUPENDA sisi kwanza.
Kama una Changamoto ya kutokuwapenda watu na kuwasamehe adui zako unahitaji msaada,
Mwombe MUNGU leo katika Kristo YESU ili akupe UPENDO WAKE ndani ya moyo wako ambao kwa nguvu yake huo utaweza kuwapenda watu wote na kuwaheshimu.
Utawasamehe adui zako na wote waliokuumiza, kuanzia hapo utaanza kuyaishi maisha ya Furaha na Amani moyoni mwako.
Naamini Atakusikia na kukusaidia ikiwa utaamua kutafuta msaada kwake kwani anasema;
Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza. #Zaburi 50:15
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. #Matthayo 11:28
wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.#Yohana 6:37
Hapo hapo ulipo,
Funika macho yako,Nyanyua mikono yako juu,Sema na MUNGU wako,Mweleze yeye unayohitaji,Mshukuru yeye kwa kukusikia na mwisho sema KATIKA JINA LA YESU KRISTO Amen!
WEWE UNAPENDWA
Reviewed by Unknown
on
5:35 PM
Rating: 5
